Share your research and experience, ask and answer questions, meet your peers.

BNFB Flyer- Ukweli kuhusu Urutubishaji kibiolojia.

Urutubishaji kibiolojia ni mchakato wa kuboresha lishe kwa kuongeza kiwango cha wingi wa vitamini na madini katika mazao ya chakula kwa kutumia njia za kawaida za uzalishaji vipando au mbegu zilizoboreshwa kupitia utafiti; utunzaji mazao shambani au matumizi ya bioteknolojia. Urutubishaji kibailojia wa mazao ya chakula ni miongoni mwa afua ambazo huchukuliwa kama ni njia mojawapo yenye gharama nafuu inayoweza kutumika na nchi mbalimbali katika kukabiliana na utapiamlo wa virutubishi vya vitamini na madini. Urutubishaji kibiolojia unawafikia walaji wa maeneo ya vijijini ambao wana uwezekano mdogo wa kupata vyakula vilivyoongezwa virutubishi kutoka katika viwanda vikubwa vya vyakula, pia kundi hilo la jamii wana uwezekano mdogo wa kupata vitamini na madini za nyongeza na kuwa na uwezo wa ulaji wa vyakula mchanganyiko. Njia ya kutumia makundi ya vyakula mchanganyiko vyenye lishe kwa wingi husaidia katika upatikanaji wa vyakula mbalimbali na huwezesha upatikanaji wa mazao yaliyorutubishwa kibiolojia katika kudhibiti matatizo ya lishe katika jamii iliyokuwa kwenye hatari ya kukosa lishe ya kutosha. Ripoti ya Dunia ya Hali ya Lishe ya mwaka 2014 (The Global Nutrition Report of 201413) inaonyesha ukubwa wa tatizo la upungufu wa vitamini A na madini chuma katika nchi za Nigeria na Tanzania.

Authors: Building Nutritious Food Baskets Project

Contributors: Joyce Maru

Pages: 2

Publication Date: January 12, 2017