Washiriki wa shamba darasa wa uzalishaji shirikishi wa viazi vitamu na udhibiti wa visumbufu vya viazi vitamu, waliomba jarida la maelekezo kuhusu ya njia mbalimbali za usindikaji wa viazi vitamu. Hii ni kwaajili ya kuwawezesha washiriki hao kukumbuka vizuri mambo waliyojifunza kwenye shamba darasa na kuboresha jitihada zao za kuendelea na mafunzo. Kwa pamoja tulijumuisha jarida la awali ambalo lilijaribiwa na washiriki wa shamba darasa 37 wa viazi vitamu, jaribio lililofanyika msimu wa 2005/06 katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania. Jarida hili la maelekezo linapatikana katika lugha ya kiswahili na kiingereza na shukrani zimwendee Dr. Regina Kapinga kwa kuandaa tafsiri ya kiswahili. Majarida mengine ni ya: Kutambua magonjwa ya viazi vitamu, wadudu adui na udhibiti wake, jarida la uzalishaji wa marando bado yanaandaliwa. Jarida hili la maelekezo linasaidia kuongezea jarida lingine la awali lililotayarishwa kwa ajili ya wawezeshaji wa uzalishaji shirikishi wa viazi vitamu na udhibiti wa visumbufu vya viazi vitamu kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara la Afrika. Jarida hili ni matokeo ya miradi ya utafiti iliyofadhiliwa na Shirikia la Ulaya la Kimataifa la Maendeleo kwa manufaa ya nchi zinazoendelea. Mambo yaliyoandikwa kwenye jarida hili sio lazima kuwa ni mawazo ya shirika la Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID). R8458 & R8167. Mpango wa Udhibiti wa afya ya Mazao.
Authors: Robert Mwanga, Sam Namanda, Tanya Stathers, Richard Gibson, Robert Mwanga, Sam Namanda, Tanya Stathers, Richard Gibson
Subjects: Utilization
Pages: 26
Publisher: Natural Resources Institute (NRI)
Publication Date: 2006