Share your research and experience, ask and answer questions, meet your peers.

Ukweli kuhusu Urutubishaji kibiolojia

Urutubishaji kibiolojia ni mchakato wa kuboresha lishe kwa kuongeza kiwango cha wingi wa vitamini na madini katika mazao ya chakula kwa kutumia njia za kawaida za uzalishaji vipando au mbegu zilizoboreshwa kupitia utafiti; utunzaji mazao shambani au matumizi ya bioteknolojia. Mifano ya vitamini na madini ambayo yanaweza kuongezwa kwa kutumia njia ya urutubishaji kibioloia ni pamoja na vitamini A inayotokana na mimea ( ), madini zinki na madini chuma.

 

Mbinu za kawaida za uzalishaji zinatumika kutambua aina ya mazao yenye virutubishi vingi vinavyohitajika. Mazao mawili yenye sifa zinazohitajika kama vile kuhimili virusi, kuhimili ukame, au kutoa mavuno mengi katika eneo husika hutumika kuzalisha aina ya zao lililo rutubishwa (kama vile vitamini A, madini chuma na zinki) pamoja na sifa nyinginezo zinazopendelewa na wakulima na walaji. Hii ni mbinu ya kawaida inayotumika zaidi katika nchi za Afrika na imewezesha kuleta mafanikio katika uzalishaji wa viazi lishe vyenye wingi wa vitamini A.

 

Kutumia agronomia ya Urutubishaji ambayo inahusisha upuliziaji wa madini kama vile madini zinki na chuma kwenye majani ya zao husika, uwekaji kwenye udongo pamoja na utunzaji mzuri wa zao, hali ya udongo na sifa za zao ili kupata ongezeko la kiwango cha virutubishi muhimu katika sehemu za zao inayotumika kwa chakula.

 

Bioteknolojia ni mchakato unaohusisha uingizaji wa jeni inayohusika na virutubishi kutoka aina moja ya zao kwenda kwenye vinasaba (DNA) vya aina nyingine ya zao linalokosa virutubishi vinavyohitajika.

Subjects: Biofortification

Pages:

Publication Date: January2017