Share your research and experience, ask and answer questions, meet your peers.

BNFB Brief- Vipando Vinne Vya Viazi Lishe Marando ya Dhahabu.

Bw. Julius Kayongola ambaye ni mkulima wa kijiji cha Ilindi alisimulia safari aliyopita hadi kuwa mzalishaji wa kuaminika wa viazi lishe na marando yake. Mwezi Desemba, 2015 mkulima huyu, alikuwa mmoja wa wanufaika wa mafunzo ya uzalishaji wa mbegu na marando ya viazi lishe yaliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Sukari cha Kibaha, Tanzania (SRI – Kibaha) kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO). Alielezea kuwa baada ya kupata mafunzo, alipewa vipando vinne vya viazi lishe kwa ajili ya kuongeza marando zaidi ambayo mpaka sasa ameshazalisha katika shamba lenye ukubwa wa nusu (1/2) eka kwa kutumia umwagiliaji. BNFB unalenga kuangalia uwezekano wa kupanua mfumo wa utekelezaji kupitia utaratibu wa vyakula mchanganyiko katika kukabiliana na njaa iliyojificha ya upungufu wa virutubishi vya vitamini na madini kwa kuhimiza uwezekaji endelevu katika kuongeza uzalishaji na matumizi ya mazao yaliyorutubishwa kibaiolojia kama vile viazi lishe, mihogo lishe (mihongo manjano), mahindi lishe (mahindi ya chungwa), na maharage lishe (yenye wingi wa madini chuma au zinki).