Share your research and experience, ask and answer questions, meet your peers.

Vipando Vinne Vya Viazi Lishe Marando ya Dhahabu

Mashamba ya kuzalishia marando ya viazi lishe yaliyopo katika kijiji cha Ilindi ni yenye kuvutia na kutia hamasa. Mashamba hayo yanaangaliwa na wazalishaji wa viazi lishe waliojitoa kwa nia moja na wanaotumia umwagiliaji kutoka katika ziwa la karibu la Manyara. Ukaribu wa mashamba na ziwa unafanya kina cha maji kiwe juu na hivyo kuwawezesha wakulima kuchimba visima vya kumwagilia mazao yao.

 

Kijiji cha Ilindi kipo katika eneo lenye ukame wa wastani katika Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma, Tanzania. Kutoka barabara kuu huwezi kuona kitu chochote cha kijani wala uzalishaji wowote; hadi utakapofika kwenye uoto wa ukijani wa mashamba mazuri ya kuzalisha marando ya viazi lishe.