Share your research and experience, ask and answer questions, meet your peers.

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu – Juzuu ya 3

Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu Kitabu cha mafunzo kwa wakufunzi cha mradi wa kuwafikia wadau wa Mabadiliko. Juzuu ya 3. Mada ya 5: Mifumo ya mbegu za viazi vitamu inapitiwa ikiwemo hatua mbalimbali za uzalishaji mbegu, na majukumu ya wadau mbalimbali katika mfumo. Sababu zinazoshawishi maamuzi ya kama kutumia mkupuo mmoja au mbinu inayoendelea ya kusambaza vipando, na viwango vya ruzuku vinavyohitajiwa pia zinaelezewa. Mifano inatolewa kwa upangiliaji wa mikakati ya uzalishaji na usambazaji wa aina mbalimbali za vipando. Mbinu za kuchagua vipando salama na kisha kuvihifadhi na kuvizalisha pia zinaelezewa.

 

 

HOW TO CITE

Stathers, T., McEwan, M., Gibson, R., Mwanga, R., Carey, E., Namanda, S., Abidin, E., Low, J., Malinga, J., Agili, S., Andrade, M., Mkumbira, J. (2013). Vyote Unavyopaswa Kujua Kuhusu Viazi Vitamu: Kitabu cha mafunzo kwa wakufunzi cha mradi wa kuwafikia wadau wa mabadiliko. 3: Vipando vya viazi vitamu. Kituo cha Kimataifa cha Viazi (International Potato Center), Nairobi, Kenya. Juzuu la 3. ISBN: 978-92-9060-429-7 DOI: 10.4160/9789290604297.v3